Mabingwa mara 7
wa michuano ya AFCON timu ya taifa ya Misri jana imefuzu hatua ya fainali ya
michuano hiyo kwa ushindi wa mikwaju ya penati 3-1 dhidi ya wenyeji Cameroon
kwenye mchezo wa nusu fainali.
Misri
wanakata tiketi ya kucheza fainali yao ya 10 ya michuano hii ya mataifa barani
Afrika wakiwa wameshinda ubingwa wa michuano hii mara 7 katika fainali 9
walizocheza mpaka sasa.
Kwenye
mchezo wa fainali watavaana na timu ya taifa ya Senegal ambao hawajawahi
kushinda ubingwa wa michuano hii na ni kwa mara ya tatu wanafuzu kucheza
fainali ya Afcon mwaka 2002, 2019 na mwaka huu 2022 mchezo wa fainaili waatacheza dhidi ya Misri kwenye fainali Jumapili Februari 6.
0 Maoni