Mwimbaji nyota wa muziki wa Rnb Robyn Rihanna Fenty maarufu kama Rihanna na mpenzi wake msanii wa Hip Hop Rakim Mayers maaruf kama A$AP Rocky wanatarajia mtoto wao wa kwanza wakiwa pamoja, wapenzi hao walithibitisha kwenye picha zilizopatikana na kwenye mtandao wa E! News.
Katika
picha hizo, zilizopigwa jijini New York mwishoni mwa wiki na kuchapishwa
Jumatatu, Januari 31, Rihanna anaonekana akionesha tumbo lake huku A$AP
akimbusu paji la uso.
Habari
hii ya ujauzito inakuja miaka miwili baada ya kuwa marafiki wa muda mrefu huku
wakihusishwa na taarifa kuwa ni wapenzi, tetesi zilizokuwepo muda mfupi baada
ya kutengana na Hassan Jameel.
Uhusiano
ulianza baada ya nyota hao kuonekana wakiwa pamoja huko New York.
0 Maoni