Viungo tegemeo hivi sasa katika kikosi cha Simba, Ousmane Pape Sakho na Sadio Kanoute wote wapo fiti na vizuri kucheza dhidi ya Ruvu Shooting.
Nyota hao wote walipata majeraha katika mchezo uliopita wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika uliochezwa wikiendi iliyopita dhidi ya Asec Mimosas ya nchini Ivory Coast.
Kurejea
kwa viungo hao kutaimarisha kikosi
hicho kinachonolewa na Kocha mkuu
Mhispania, Pablo Franco na msaidizi wake, Selemani Matola.
Simba inacheza na Ruvu Shooting leo Februari 16, kwenye mchezo wa hatua ya 16 bora ya kombe Azam Sports Federation Cup uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es salaam.
0 Maoni