Kiungo Mshambuliaji wa Simba Pape Ousmane Sakho, amechaguliwa mchezaji bora wa mashabiki wa mwezi Januari (Emirate Aluminium ACP Simba Fans Player of the Month).


Sakho raia wa Senegal amewapiku nyota wenzake wawili Sadio Kanoute wa Mali na Henock Inonga wa DRC ambao aliingia nao fainali.

Katika mwezi Januari Sakho amecheza mechi saba akidumu uwanjani dakika 563 na amefunga mabao matatu huku akionyesha kiwango safi.

Kwa ushindi huo Sakho atakabidhiwa fedha taslimu Sh 2,000,000 na tuzo kutoka kwa wadhamini wa tuzo hizo.

Mchanganuo wa kura zilivyopigwa

Pape Sakho – 58.02% (1015)

Henock Inonga – 34.67% (607)

Sadio Kanoute – 7.31% (128)

Chanzo> Simba.