Ikiwa zimepita siku mbili tangu timu ya taifa ya Misri ipoteze mchezo wa fainali dhidi ya Senegal, staa wa
Liverpool Mohamed Salah ameanza mazoezi leo Februari 8, kujiwinda na michezo ya ligi kuu
England.
Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amesema kuna uwezakano mkubwa wa Salah kucheza katika mchezo wa Epl dhidi ya Leicester City Alhamisi, kuhusu
Mane, Klopp amesema uwezakano wa kucheza haupo maana bado hajaripoti kambini.
Salah hakupiga mkwaju
ya penati kwenye mchezo wa fanaili jumapili ambayo walipoteza
huku Mane akipiga Penati ya ushindi kwa Senegal.
0 Maoni