Timu ya taifa ya Senegal imetwaa ubingwa wa michuano ya AFCON kwa mara ya kwanza katika historia kwa mikwaju ya penati 4-2 dhidi Misri ambao ni mabingwa mara 7 wa michuano hiyo kwenye mchezo wa fainali uliochezwa katika uwanja wa Olembe Yaoundé Cameroon.
Timu hizi zilifikia hatua
ya kupigiana mikwaju ya penati baada ya kucheza dakika 120 ambazo zilimalizika
kwa suluhu 0-0, kwenye penati hizo Sengeali walifunga peanati 4 kati ya 5
walizopiga, Misri walikosa penati 2 kati ya 4 walizopiga hivyo Senegal wakaibuka
kwa ushindi wa penati 4-2.
Huu ni ubingwa wa kwanza
kwa Senegal katika fainali 3 walizocheza kwenye nichuano hii ya mataifa barani
Afrika, Fainali ya kwanza walicheza mwaka 2002 walifungwa na Cameroon kwa
mikwaju ya penati 3-2, na fainali ya pili walicheza mwaka 2019 wakafungwa na
Algeria bao 1-0, na jana ilikuwa ni fainali yao ya na tatu na ya pili
mfululizo.
Misri ambao ni mabingwa
mara 7 na wamepoteza fainali yao ya 3 katika fainali 10 walizocheza na mara ya
mwisho kutwaa ubingwa wa michuano hii ilikuwa mwaka 2010 ambapo waliifunga
Ghana mabo 1-0 kwenye mchezo wa fainali.
Sadio Mane wa Senegal
ametajwa kuwa mchezaji bora wa mashindano, golikipa wa Senagal Edouard Mendy
amechagiliwa kuwa kipa bora na mshambuliaji wa Cameroon Vincent Aboubakar
amemalizi akiwa kinara wa ufungaji akopachika na mabao 8.
0 Maoni