Kuelekea mchezo wa kesho ligi kuu ya NBC kati ya bingwa mtetezi Simba  dhidi ya Tanzania Prisons, kocha msaidizi wa  Seleman Matola amesema wataendelea kumkosa kiungo wao Jonas Mkude na  kungo mshambuliaji Kibu Dennis bado hawajwa fiti  kwa asilimia 100 kuanza kucheza mechi baada ya  kuumia.




Akiongea kwenye mkutano na waandishi wa habari leo Februari 2, Matola amesema licha ya kuachwa kwa pointi 10 bado wana matumaini ya kuendelea kutetea taji hilo"tofauti ya alama 10 ni nyingi kwa timu inayotaka ubingwa wa lakini tutaendelea kupambana kupata alama 3 kwenye mechi zote ili tutetee taji letu." 



Ikumbukwe Simba wataendelea kumkosa Kocha wao mkuu Pablo Franco anatumikia adhabu ya kufungiwa mechi tatu na bodi ya ligi .


Simba inashuka dimbani kesho dhidi ya Tanzania Prisons ya Mbeya kwenye dimba la Benjamin Mkapa Dar es Salaam saa 1:00 usiku.