Klabu ya Simba itawakosa nyota wake watano katika mchezo wa kombe la Shirikisho Barani Afrika Jumapili Februari 13, dhidi ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast.





Kocha wa Simba Sc Pablo Franco amesema miongoni mwa wachezaji hao ni Chris Mugalu ambaye amevunjika mkono.


Pablo hajaweka wazi kuhusu undani wa jeraha hilo la Mugalu ila ameeleza kuwa ataukosa mchezo dhidi ya ASEC Mimosas.


Nyota wengine ni Bernard Morrison ambaye amesimamishwa na klabu hiyo, Kibu Denis na Thadeo Lwanga ambao bado ni majeruhi.



Mchezaji mwingine ambaye ataukosa mchezo huo ni 
Clatous Chota Chama ambaye haruhusiwi kushiriki mashindano hayo kwa mujibu wa kanuni za Shirikisho la soka Barani Afrika kwa sababu ameochezea RS Berkane ya Morocco.