Ni Simba dhidi ya Tanzania
Prisons leo Februari 3, mechi ya Ligi kuu NBC ambayo huwa inavuta hisia za
wapanda kandanda hapa nchini.
Msimu uliopita wajela jela
walifanikiwa kuondoka na alama nne mbele ya Simba wakishinda na kutoa droo japo
Simba alibeba ndoo ya ligi kuu.
Wote wametoka kupoteza
michezo yao ya mwisho na hata ubora wao msimu huu unaonekana kidogo kushuka na
kuifanya mechi ya leo kuzidi kuwa ngumu.
Simba wametoka kupoteza michezo miwili ya Ligi
Kuu, leo hii watataka kutafuta alama tatu ili kupunguza alama kati yake na anayeongoza
msimamo wa Ligi.
Tanzania Prison wakiwa wanashika mkia kwenye msimamo
nao wanatafuta alama tatu muhimu kwao kujikwamua sehemu waliopo wakiwa alama 11
baada ya kushuka dimbani mara 13, imepoteza michezo nane na ina sare mbili.
Simba watataka kurudisha ari ya ushindi ili
wachezaji warudishe hali ya kujiamini kwenye kikosi chao kabla ya mchezo wa
kombe la shirikisho.
Majibu ni leo saa 1:00
usiku katika dimba la Benjamin Mkapa.
0 Maoni