Klabu ya Simba imesema aliyekuwa mdhamini mwenza wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara (NBC Premier League), GSM wamejitoa katika udhamini huo kutokana na Simba kutokubaliana na matakwa ya mkataba huo walioingia na Bodi ya Ligi.
Haya yamesemwa na Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally;pamema leo akiwa kwenye kipindi cha michezo cha Sports Arena cha Wasafi Fm “Kwanza tuwapongeze TFF kwa kutuletea wadhamini maana ni jukumu la kila Klabu kutafuta mdhamini wake lakini sijui ni masoko yamekuwa magumu vilabu havipati hao wadhamini lakini isitumike kama fimbo ya kutuletea kila aina ya mdhamini.
“Kwa wakati ule hawakutuelewa lakini hatimaye jana wametuelewa na baada ya kutuelewa ndio tukasema “HAKI IMESHINDA sisi tulikuwa tunapigania haki na haki hiyo imeshinda.
“Simba hatukukubaliana na ule mkataba tangu mwanzo Kwasababu tuliona hauna viashiria bora kwenye maslahi ya mpira wetu na tulijaribu kupambana lakini bahati mbaya wenzetu hawakutuelewa kwa maana ya vilabu na hii ndio shida kubwa ya mpira wetu.
0 Maoni