Bingwa mtetezi wa ligi kuu ya NBC Simba,leo Februari 3 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa Dar, imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wajela jela Tanzania Prisons.

 

Goli pekee la Simba limefungwa kwa mkwaju wa penati na mshambuliaji Meddie Kagere dakika ya 67 baada ya beki wa Prisons kuunawa mpira ndani ya 18.

 

Simba ambayo ilianza viungo wengi iliafanikiwa kumiliki mpira ambao haukuwa na madhara kwenye lango la Prisons ambao waliamua kupaki basi na kucheza mpira ya kushtukiza ambayo ilionekana kuwa ya hatari langoni mwa Simba.

 

 Iliwachukua Simba dakika 67, kupiga mpira  uliolenga lango (shot on target) ambao ni mkwaju wa penati ya Kagere.

 

Baada ya mchezo kocha msaidizi wa wekundu wa msimbazi Suleman Matola, amesema hajaridhika na ushindi kiduchu walioupata lakini amekiri ni nguma kucheza na timu kama Prisons ambayo muda mwingi wanazuia.

 

Mnyama Simba amefikisha alama 28 baada ya michezo 14, Yanga inaongoza msimamo wa ligi  na alama 35.