Klabu ya Simba leo Februari 10, imetambulisha jezi mpya zenye nembo ya Visit Tanzania ambazo zitatumika kwenye hatua ya makundi ya kombe la shirikisho barani Afrika.
Akizungumza Mtendaji Mkuu wa Simba Barbara Gonzalenz amesema kwenye mashindano ya Afcon yaliofanyika Cameroon Simba inazungumziwa kikubwa hivyo waneona haja ya kurudi tena na Visit Tanzania
"Nilipokuwa AFCON nimegundua Simba inaheshimika sana nje ya nchi yaani inazungumzwa kiukubwa mno, wanawafuatilia hadi profile za wapiga picha wetu.
Na kwa mantiki hiyo msimu huu kwenye mashindano ya CAF kama klabu tumeona tuipeperushe bendera yetu 🇹🇿 kwa kuendelea kutumia neno Visit Tanzania"
Amesema
uzi huo utaanza kuuuzwa kuanzia kesho katika maduka ya Vunja bei na Sandaland
Only One, na kuwataka mashabiki kununua kwa wingi jezi hizo.
"Leo tunaonyesha jezi
yetu ya michuano ya kimataifa ikiwa na logo ambayo inazingatia mambo yote ya
utalii, jezi zitaanza kuuzwa kesho kwenye maduka ya Vunja Bei na Sandaland the
Only One."- Amesema Barbara.
Naye mwenyekiti wa bodi ya
utalii Jaji Mstaafu Thomas Mihayo amesema Simba inapovaa Visit Tanzania
inahamasisha watanzania kutembelea vivutio mbalimbali
"Jambo lolote ambalo lina maslahi kwetu kama Bodi ya Utalii lazima tulipe ushirikiano, lazima tulishangilie.
"Simba inapovaa jezi zimeandikwa Visit
Tanzania imekuwa na faida sana. Kuvaa jezi hizo kumehamasisha Watanzania na
kumekuwepo na ongezeko la watalii kutoka nje ya nchi."- Mwenyekiti wa Bodi
ya Utalii Tanzania (TTB), Jaji Mstaafu Thomas Mihayo
0 Maoni