Bingwa mtetezi wa kombe la Azam Sports Federation Cup Simba imefanikiwa
kuingia hatua ya robo fainali ya michuano hiyo kibabe baada ya kuibuka na
ushindi wa mzito wa mabao 7-0 dhidi ya Ruvu Shooting, mechi iliyochezwa leo
usiku Februari 16 uwanja wa Benjamin Mkapa Dar.
Katika mchezo nyota wa Kimataifa wa Zambia Cloutus Chmama
ameondoka na mpira baada ya kufunga magoli matatu Hat Trick akifunga kwenye
dakika ya 25’ 28 na 75, huku mshambuliaji Rafael Bocco akifunga mabao mawili dakika
ya 2 na 40.
Beki wa Ruvu Shooting aliwazadia bao Sib baada ya kujifunga
katika kipindi cha kwanza dakika ya 44 ya mchezo, Jimmyson Mwanauke naye
akitokea benchi aliiandikia simba bao dakika ya 70 .
0 Maoni