Hatimaye Mason Greenwood ameachiwa kwa dhamana leo Februari 2, baada ya kushikiliwa na polisi siku tatu kwa tuhuma za unyanyasaji wa kingono na vitisho vya kuua.

 


Klabu ya Manchester United imeweka wazi kuwa mchezaji huyo hataruhusiwa kuichezea au kufanya mazoezi na kikosi hicho wakati polisi bado wakiwa wanaendelea na uchunguzi.

 

Mastaa kadhaa wa klabu hiyo wame ‘mu unfollow’ Greenwood kwenye kurasa zao za mitandao ya kijaamii kufuatia tuhuma hizo.

 

 Greenwood, 20, alikamatwa kwa tuhuma za ubakaji na shambulio baada ya video na sauti kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii zikimuonyesha anayedauwa jywa mpenzi wake akiwa anavuja damu usoni baada  kupigwa.