Tanzania imeporomoka kwa nafasi moja katika viwango vya ubora wa soka vya Shirikisho la Mpira wa Miguu Dunia (FIFA) kwa mwezi Januari.
Kwa mujibu wa viwango vya ubora wa soka vya Januari vilivyowekwa hadharani jana, Tanzania imeanguka kutoka nafasi ya 131 iliyokuwepo mwishoni mwa mwaka jana hadi nafasi ya 132 ikipishana na Comoro ambayo awali ilikuwa katika nafasi hiyo.
Kufanya vizuri kwa Comoro katika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zilizofanyika huko Cameroon mwaka huu, kuimeirudisha nchi hiyo katika nafasi ya 131 na kuichomoa Tanzania ambayo haikushiriki.
Gambia ambao walionyesha kiwango bora na kuishia katika hatua ya robo fainali kwenye fainali za Afcon mwaka huu, juhudi zao zimewalipa kwani imejikuta ikipanda kwa nafasi nyingi na kuwatoa shimoni walipokuwepo awali.
0 Maoni