Aliyekuwa  mchezaji wa Ruvu Shooting, Ally Mtoni "Sonso" (29) amefariki Dunia leo  katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa anapatiwa Matibabu.



Taarifa za awali zinasema kuwa, Sonso ambaye alikuwa beki wa kushoto alikuwa akiugua maradhi ya 
alikuwa akiuguza majeraha ya mguu tangu Oktoba mwaka jana.


Kwa nyakati tofauti, Sonso 29 amezitumika timu za Lipuli FC, Yanga SC, Kagera Sugar, Polisi Tanzania. pia amewahi kucheza timu ya Taifa.


Katika salamu zake za Pole klabu ya Yanga imesema wanamkumbuka Sonso kwa mengi ikiwemo Ujasiri wake  ndani ya Uwanja, nidhamu pamoja na kujitolea kuipigania jezi ya klabu hiyo.