Kiungo fundi wa Kidachi Donny van de Beek ametimkia
Everton akitokea Manchester United kwa mkopo mpaka mwisho wa msimu.
Donny ambaye amekuwa akisota benchi tangu kwa muda mrefu
ameicheza United mechi 50 tu katika miaka miwili ya kocha alitimuliwa Ole
Gunner Solskjaer, na meneja wa muda wa sasa Ralf Rangnick.
“Nimekuwa na mazungumzo mazuri na kocha Lampard
tumejadili mambo mengi kuhusu mpira na tuna malengo yanayofanana na amechangia
sana maamuzi yangu ya kuja hapa Everton”
“Nimecheza nae nikiwa Ajax yeye akiwa kocha wa Chelsea ananijua
vizuri kiuchezaji naamini ninao uwezo kuisadia timu” ameongeza Donny.
Van de Beek atakuwa akivaa jezi namba 30, atalipwa mshahara wa paundi 100,000 kwa wiki ambazo Everton watakuwa wakimlipa na haitaruhisiwa kusajiliwa moja kwa moja na timu hiyo pale mkataba huo wa mkopo utakapoisha.
0 Maoni