KATIKA kuhakikisha wanapata ushindi wa kwanza nyumbani dhidi ya Asec Mimosas ya nchini Ivory Coast katika mchezo wa kwanza wa makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, Rais wa Heshima wa Simba, bilionea Mohamed Dewji ‘Mo’, ameahidi kuwapa bonasi nzuri inayofikia Sh 200Mil kama wakifanikiwa kuwafunga wapinzani wao hao.
Mo juzi alotinga kwenye kambi ya timu hiyo iliyopo Bunju, nje kidogo ya Dar es Salaam, saa chache kabla ya kuelekea mazoezini kwa ajili ya kuzungumza na wachezaji hao.
Mara baada ya kuvamia kambini hapo alifanya kikao na wachezaji, benchi la ufundi na viongozi wakiwemo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya timu hiyo, Salim Abdallah ‘Try Again’,Mtendaji Mkuu, Barbara Gonzalez na mjumbe wa bodi, Mramu Ng’ambi.
Timu hizo zinatarajiwa kuvaana Jumapili hii saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.
0 Maoni