Siku moja baada ya idara ya Habari ya Yanga kufanya mkutano na waandishi wa habari, kueleza malalamiko yao kuhusu uendeshaji wa ligi, leo Februari 9,  wazee wa klabu hiyo nao wamefanya mkutano na waandishi kusisitiza kwamba wameandika barua ya kuomba kukutana na Mh. Rais Samia Suluhu Hassan, kwenda kushtaki maovu ya TFF.


              


Wazee hao wa klabu ya Yanga wamesema kuwa wamechoshwa na mwenendo wa waamuzi wa Tanzania na wanataka mpira uchezeshwe kwa haki.



Ikiwa uonevu ukiendelea dhidi ya Yanga wazee wa klabu hiyo wamesema watakwenda mahakamani ili kusitisha ligi.



Pia wazee wamedai kuwa kama kuna bingwa ameandaliwa apewe kombe ili wao waendelee na mambo mengine.