Waziri wa Fedha na Mipango Mwigulu Nchemba amesema atakaa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohammed Mchengerwa ili waongee uwezekano wa kutenga bajeti ya kununua VAR na nyasi bandia.



Hatua hiyo imekuja baada ya Goli la Fiston Mayele katika mchezo kati ya Yanga dhidi ya Mbeya City kukataliwa kwa madai kuwa alikuwa ameotea.


Nitashauriana na Waziri mwenzangu anayesimamia Michezo bajeti ijayo tumtafutie Fedha, Tuweke VAR viwanja hata 10, tuweke nyasi bandia kuondoa utaratibu wa kucheza football shambani. Haya ndio maeneo yanayolalamikiwa. Otherwise Yanga jana, they deserved a win, were denied a win.