Klabu ya Yanga imesema kuwa hairidhishwi na baadhi ya maamuzi ambayo yanonekana kuipendelea Simba na kuongeza kuwa viongozi hawatoi malalamiko kwa Waamuzi ila huwa wanafanya hivyo kuwakumbusha tu.
Hayo yamesemwa na Ofisa Habari Hassan Bumbuli na Msemaji wa klabu hiyo Haji Manara mbele ya waandishi wa Habari leo Februari 8, 2022
Haji Manara amesema kuwa wajibu wao ni kukumbusha tu, ila sio kupeleka malalamiko kwa waamuzi kwa kuwa klabu yao ina mashabiki na wanaona kuwa Haki Haitendeki na wao kazi yao ni kusema kwa kuwa ndio kazi ambayo wameichagua.
“Nilisema pale EFM hatuchezi ligi hii kuwa unbeaten tunacheza kuwa champion, Sisi ni klabu ya mpira lazima tutafungwa. ni wenzetu tu ambao wanaamini wakifungwa wamehujumiwa.
“Sisi tunajua hii ni klabu ya mpira lazima kuna siku utapigwa.”
Naye Ofisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema kuwa katika michezo 14 ambayo klabu ya Young Africans ilicheza kwenye ligi kuu Msimu huu, walibahatika kuongezewa dakika 34 tu (Jumla) ikiwa na mgawanyiko wa ongezeko la dakika 2,3 mpaka 5 wenye michezo 15 ambayo klabu ya Simba iliyocheza kwenye ligi msimu huu, waliongezewa dakika 75 ikiwa na mgawanyiko wa ongezeko la dakika 4, 5 mpaka 7.
“Tunataka waamuzi wetu waanze kujitafakari juu ya
haya ambayo yamekuwa yakiendelea na yamekuwa mjadala mkubwa sana kwenye taifa
letu, lakini pia tunataja mamlaka zinazosimamia mpira zichukue hatua juu ya
jambo hili ambalo watu wamewekeza pesa zao.

0 Maoni