Vinara wa Ligi kuu Yanga
wanashuka dimbani leo Februaru 5 majira ya saa 1:00 usiku uwanja wa Benjamin
Mkapa kuwakaribisha Mbeya City.
Yanga ambayo haijawahi
kupoteza mchezo dhidi ya Mbeya City katika misimu minne mfululizo iliyopita
tangu mwaka 2017, ikishinda mara nne na kutoka sare mara nne.
Wananchi wanakutana na
Mbeya City ya tofauti ikiwa ikiwa imejikusanyia alama 22, imepoteza mchezo
mmoja kati 13 walipoteza dhidi ya Coastal Union walifungwa mabao 3-2 na
ina sare saba.
Licha ya kufunga magoli 17
lakini safu ya ulinzi imeruhusu magoli 11 na leo Mbeya City watakuwa na kibarau
kigumu cha kuizua safu bora ya ushambuliaji
msimu Yanga imetikisa wavu wa wapinzani mara 23.
Je Mbeya City watafanikiwa kuizua Yanga ambayo iko kwenye kiwango bora kwa sasa wakiwa na safu ya ushambuliaji hatari ikiongozwa na Fiston Mayele? Majibu ni saa 1:00 Usiku.
0 Maoni