Vinara wa ligi kuu ya NBC,Yanga ikiwa katika dimba la
nyumbani Benjamin Mkapa leo Februari 5, imelazimishwa Suluhu na Mbeya City hii ni ya tatu msimu huu kwenye mechi za Ligi.
Mbinu za Mbeya City kocha Mathias Lule zimeonekana
kuwasumbua Yanga katika akiafanikiwa kuibana Yanga eneo kiungo na kuwafanya
Khalid Aucho Gift Mauya kushindwa kucheza kwa UUhuru
Uimara wa mlinda mlango wa Mbeya City Deogratis Munisgi ‘Dida’
umeunyima ushindi Yanga baada ya kuokoa mpira wa Chiko ushindi dakika za lala
salama.
Yanga imeendelea kubaki kileleni na alama 36 huku Simba
amabayo inshuka dimbani kesho ina alama 28 na kama watashinda watapunguza alama
na kubaki tano.
0 Maoni