Yanga  imefanikiwa kwenda Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada kuibuka na  ushindi wa 2-1 dhidi ya Biashara United jana usiku mchezo uliopogwa  Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.





Mabao ya Yanga SC yote  yamepachikwa na nyota kutoka DRC, beki Yannick Litombo Bangala dakika ya 22 na mshambuliaji Fiston Mayele dakika ya 28, wakati la Biashara United limefungwa na  Mkenya, Collins Opare dakika ya 38.

 

Polisi Tanzania ilifanikiwa pia kwenda Robo Fainali  baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya wenyeji, Tanzania Prisons mabao ya Said Khamis dakika ya 40 na Daruwesh Saliboko dakika ya 83 Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.