Uongozi wa Yanga, umezima tetesi za kuondokewa na baadhi ya wachezaji wake ambao mikataba yao inatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu kwa kusema hao wanaowahitaji wanajisumbua na badala yake mastaa hao wataendelea kukipiga Jangwani.
Baadhi ya wachezaji wa Yanga ambao mikataba yao inatarajiwa kumalizika mwisho wa msimu huu ni nahodha Bakari Mwamnyeto anayetajwa kuwaniwa na Simba.
Wengine ni Dickson Job, Kibwana Shomari, Saidi Ntibazonkiza ‘Saido’, Yacouba Songne, Deus Kaseke na Abdallah Shaibu ‘Ninja’ ambaye hivi karibuni alipelekwa nchini Tunisia kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji wa goti.
Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Spoti Xtra, kutoka kwa mmoja wa mabosi wenye ushawishi ndani ya timu hiyo, alisema wachezaji hao wameshamaliza mazungumzo ya awali kwa ajili ya kuongeza mikataba kuendelea kukipiga Yanga.
Chanzo>SpotiXtra.
0 Maoni