Nyota wa Kimataifa wa Morocco Hakim Ziyech ametangaza
kustaafu kuichezea timu ya taifa hiyo baada ya kutoa kwa mgogoro na kocha Vahid
Halilhodzic.
Halilhodzic hakumjumuisha Ziyech kwenye kikosi kilichoshiriki
michuano ya AFCON iliyomalizika Jumapili hii nchini Cameroon.
Staa huyo wa Chelsea alituhumiwa kocha wake kuwa alidanganya kuwa ni majeruhi ili asicheze timu
ya taifa, mara ya mwisho kuitwa kwenye kikosi cha Simba wa Atlas ilikuwa June 2021.
Akiwa Abu Dhabi Falme za Kiarabu akijiandaa na mechi za Klabu
Bingwa ya Dunia akiwa na klabu ya Chelsea Ziyech amesema anajua kuwa uamuzi wake utawaumiza mashabiki lakini budi kuchukua maamuzi hayo.
0 Maoni