Beki wa timu ya  West Ham United  ya Uingereza Kurt Zouma, anaweza kufunguliwa mashtaka baada ya kurekodiwa kwenye picha ya video akmpiga paka wake kama mpira kwenye sakafu ya jikoni yake.





Kwenye video hiyo  pia anaonekana kumpiga kofi usoni paka huyo, klabu imelaani kitendo chake na "itashughulikia suala hilo ndani".


Zouma anaonekana akimshambulia mnyama huyo kwenye jumba lake la kifahari la pauni milioni 2 huku kaka yake akichukua video .

.

Jana usiku, Zouma aliomba radhi kwa shambulio ambalo limekosolewa vikali kwenye mitandao ya kijamii na kwa watetezi wa haki za Wanyama.