Mabingwa wa watetezi wa ligi kuu ya NBC Simba jana usuku ilifanikiwa kuondoka na alama tatu dhidi ya Dodoma Jiji, baada ya kuichapa kwa mabao 2-0 mchezo uliochezwa kwenye uwanja Benjamin Mkapa Dar es salaam.

Kiungo mshambuliaji wa Simba Clatous Chama Akishangilia baada ya kufunga goli la kuongoza dhidi ya Dodoma Jiji.


Magoli ya Simba yalifungwa Clatous Chama dakika ya 57 kwa makwaju wa penalti na kumfanya sasa kufikisha magoli matatu akicheza mechi sita tangu arejee tena Msimbazi.


Goli la pili lilizamishwa na mshambuliaji Meddie Kagere dakika ya 75’ akiunganisha vema krosi ya Peter Banda, Kagere sasa anafikisha magoli 6 kwenye ligi ya NBC.

Rally Bwalya akimpongeza Meddie Kagere baada ya kukamisha bao la pili dhidi ya Dodoma Jiji

Kwa matokeo ya Jana Simba sasa imefikisha pointi 37 baada ya kushuka dimbani mara 17, Yanga inaongoza ligi hiyo kwa alama 45.