KOCHA Mkuu wa Simba, Pablo Franco, ameweka wazi kuwa kuelekea mchezo wao wa Jumapili dhidi ya RS Berkane, benchi la ufundi la timu hiyo linafanya maandalizi makubwa kuhakikisha si tu kwamba kikosi chao kinaibuka na ushindi dhidi ya Berkane, lakini pia kinatoa burudani ya kibingwa.



Simba wanatarajia kuvaana na Berkane kesho Jumapili katika mchezo wao wa nne wa hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika, ambapo mpaka sasa wamefanikiwa kukusanya pointi nne katika michezo yao mitatu ya awali wakishinda mchezo mmoja, sare mchezo mmoja na kupoteza mchezo mmoja.

Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara kwenye kundi lao D, wakishika nafasi ya pili kwenye msimamo na pointi zao nne, huku RS Berkane wao wakiwa ndio vinara wa msimamo na pointi zao sita walizokusanya katika michezo mitatu.