Muigizaji wa Marekani Jussie Smollett amehukumiwa kifungo cha siku 150 jela baada ya jopo la mahakama kugundua kuwa alidanganya polisi kuhusu madai yake ya kuathiriwa kwa uahalifu na chuki.
Nyota huyo wa zamani wa Empire, mwenye umri wa miaka 39, alipatikana na hatia mwezi Desemba kwa mashtaka matano ya kufanya fujo baada ya kutoa taarifa za uongo kuhusu shambulio hilo la uwongo.
Adhabu hiyo pia inajumuisha miezi 30 ya muda wa uangalizi na sambamba na kulipa faini ya Dola za Marekani 145,000 sawa na zaidi ya Sh milioni 300 za kitanzania.
Kesi hiyo ilitokana na tukio la miaka mitatu iliyopita ambapo Smollett alisema alishambuliwa na watu wawili.
Muigizaji huyo alisema washambuliaji walimzomea na wakamtupia " kemikali" na kumfunga kitanzi shingoni alipokuwa akitembea usiku wa manane Januari 2019.
Mamlaka ilifungua uchunguzi, lakini mnamo Februari mwaka huo, polisi walimshtaki Smollett kwa kuwasilisha ripoti ya uwongo kwa polisi, akidai alikuwa amefanya shambulio hilo.
0 Maoni