Shirikisho la mpira wa Miguu Ulaya (UEFA) limeanza uchunguzi dhidi ya Mtendaji Mkuu wa PSG, Nasser El Kherafi na Mkurugenzi wa Ufundi, Leonardo juu ya tuhuma za kufanya fujo baada ya filimbi ya mwisho kwenye mchezo kati ya Real Madrid na PSG.
Inadaiwa wawili hao walienda vyumbani kuwaghasi Waamuzi wa mchezo huo wakilalama kuwa hawakuwa sahihi kwenye maamuzi haswa bao la Benzema, ikisemakana alimchezea rafu Gigi Donnaruma.
Katika mchezo huo PSG ilitupwa nje ya
michuano hiyo kwa jumla ya mbao 3-2 ambapo katika mchezo huo ilipoteza kwa
magoli 3-1.
0 Maoni