Mnyama Simba anaingia mawindoni leo Novemba 16, 2022 kuiwinda Namungo Fc katika mchezo ligi kuu ya NBC utakaopigwa uwanja  wa Benjamin Mkapa majira ya 1:00 usiku.


 

Namungo inaingia kwenye mchezo huu ikiwa na kumbukumbu mbaya mbele ya Simba, tangu ipande daraja msimu wa 2019 na kuanza kucheza ligi kuu haijawahi kuifunga Simba.

Timu hizi zimekutana kwenye michezo 6 ya ligi kuu, Simba imeshinda mechi 4 wametoka sare mara 2 huku Simba ikifunga magoli 13 na anmungo wakifunga magoli 5.


 

Simba ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ikiwa na alama 21 baada ya kushuka dimbani mara 10 na Namungo Fc ipo nafasi ya sita na alama 15 ikicheza ichezo 10.