Klabu ya Chelsea ya England imepanga kuanza mazungumzo na kocha wa zamani wa Barcelona na Timu ya Taifa ya Hispania Luis Enrique.
Enrique amesafiri leo kuelekea jijini London Uingereza kwa
ajili ya mazungumzo na 'The Blues' ili aweze kuwa Kocha wa klabu hiyo.
Kocha wa zamani wa Barcelona Luis Enrique
Hivi karibuni Chelsea walimfukuza kazi kocha Graham Potter baada ya kuwa na mfululizo wa matokeo mabaya kwenye ligi kuu ya England na Ligi ya Mabingwa Ulaya.
The blues pia wanahusishwa na Julian Nagelsmann ambaye wiki iliyopita alifukuzwa
kazi katika kalbu ya Bayern Munich ya Ujerumani.

0 Maoni